UDART

UDA RAPID TRANSIT PLC

UDA RAPID TRANSIT PLC

Alert GIF Mkurugenzi Mkuu Udart Waziri Kindamba Atembelea Vituo Kuona Hali Ya Huduma.

Mkurugenzi Mkuu wa UDART,  Waziri Kindamba leo tarehe 18/06/2024 alifanya  ziara na kutembelea vituo vya huduma za Usafiri zinzotolewa na UDART, hii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu na kutaka kujikita zaidi katika maboresho ya huduma za usafiri zinazotolewa na Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART.

Mkurugenzi Mkuu,  Waziri Kindamba, alianza ziara yake kwa kupitia sehemu za miundombinu  ya huduma za BRT ili kuweza kutambua  changamoto za usafiri barabarani ambazo mara nyingi zinawakuta Madereva wa Mabasi yaendayo haraka UDART ikiwemo watumiaji wa vyombo binafsi vya usafiri katika miundombinu ya BRT wasio rasmi (Madereva wa pikipiki za abiria Bodaboda na magari bisnafsi yanayopita katika miundombinu ya BRT).

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu pia ililenga kufuatilia utoaji huduma katika vituo vya BRT na kuzungumza moja kwa moja na abiria ili kupata maoni yao kuhusu huduma. Mazungumzo  hayo vilevile yalilenga kuelewa vizuri changamoto zinazowakabili abiria na kujua jinsi huduma zinavyoweza kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa huduma za Mabasi yaendayo haraka.

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu, Waziri Kindamba ilijumuisha ukaguzi wa huduma katika vituo kadhaa muhimu vya BRT katika jiji la Dar es Salaam. Miongoni mwa vituo alivyotembelea ni pamoja na Kituo Kikuu cha abiria cha Kimara (Kimara BRT Bus Terminal). Kituo cha abiria cha Kimara ni moja kati ya vituo vya BRT vinavyo hudumia  idadi kubwa ya abiria kila siku. Mkurugenzi Mkuu Waziri Kindamba alifika Kimara Terminal mapema asubuhi ili kushuhudia shughuli za huduma za asubuhi na kuona jinsi abiria wanavyopata huduma za usafiri.

Mkurugenzi Mkuu katika ziara hiyo alizungumza na abiria waliofika mapema katika Kituo kikuu cha abiria cha Kimara. Aliweza kusikiliza maoni ya abiria kuhusu huduma za usafiri, ikiwa ni pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika safari zao za kila siku. Abiria walitoa maoni yao kuhusu muda wa kusubiri mabasi, ubora wa mabasi  na changamoto za  kihuduma, na ushauri jinsi ya kuboresha mfumo mzima wa usafiri wa huduma za UDART katika vituo vya BRT.

Moja ya mambo muhimu katika ziara ya Mkurugenzi Mkuu ilikuwa ni kuchukua maoni ya moja kwa moja kutoka kwa watumiaji wa huduma za BRT, baada ya kuzungumza na abiria alipata muda wa kujadiliana na timu ya usimamizi wa huduma za UDART ili kutambua mapendekezo yaliyotolewa na abiria na njia bora za kutekeleza maboresho ya huduma, pia kuona umuhimu wa kuzingatia maoni ya watumiaji katika maamuzi ya kuboresha huduma za usafiri zinazotolewa na Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART.

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu  Waziri Kindamba katika vituo vya BRT vinavyotumiwa kwa huduma na Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka ni hatua muhimu katika juhudi za UDART za kuboresha huduma za usafiri jijini Dar es Salaam. Kupitia mazungumzo na abiria na ufuatiliaji wa changamoto za miundombinu ya huduma ikiwemo barabara za BRT, alipata ufahamu wa kina kuhusu changamoto zinazokabili huduma na jinsi ya kuzitatua ili kuimarisha huduma kwa abiria na kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa na UDART.

Share With Friends

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

Recent Posts

Scroll to Top