UDART

UDA RAPID TRANSIT PLC

UDA RAPID TRANSIT PLC

Alert GIFSemina ya Mafunzo kwa Vitendo ya Zimamoto kwa Madereva wa UDART na Wafanyakazi wa Idara zingine UDART.

Madereva wa Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam UDART pamoja na wafanyakazi kutoka idara mbalimbali wamehudhuria semina muhimu ya kuzima moto iliyoandaliwa katika ofisi mpya za Udart zilizopo Ubungo. Semina hiyo iliyofanyika tarehe 20 Juni 2024 imeonekana kuwa fursa nzuri kwa wafanyakazi hao kujifunza stadi mpya za kukabiliana na hatari ya moto na jinsi ya kuepuka majanga yanayoweza kutokea kutokana na moto.

Semina hii ya mafunzo ilikuwa ni sehemu ya maagozo na uwezeshaji wa MKURUGENZI MKUU wa UDART Waziri Kindamba ikiwa pia ni sehemu ya kuhakikisha uimarishaji wa uwezo  kwa wafanyakazi na huduma zinazotolewa na Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART.

Semina hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi kutoka idara mbalimbali za Udart, ikiwemo madereva wa Udart ambao mara kadhaa wanakutana na hatari ya moto katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Pamoja na kuwajumuisha madereva, semina hiyo pia iliwashirikisha wafanyakazi kutoka idara zote za Kampuni ya UDART na pia ngazi ya utawala.

Moja ya mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo ilikuwa ni jinsi ya kuzima moto kwa usalama na kwa haraka, hasa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira ya ofisi au vituo vya abiria vinavyotumiwa kutoa huduma na Udart. Washiriki walipata mafunzo ya vitendo jinsi ya kutumia mitungi ya gesi ya kuzimia moto, na pia jinsi ya kuwa na mkakati wa kuondoka katika majengo kwa usalama wakati wa moto.

Wakizungumzia mafunzo waliyoyapata, baadhi ya washiriki walielezea kuridhishwa kwao na jinsi semina hiyo ilivyokuwa na manufaa kwao. Baadhi ya madereva wa UDART waliohudhuria semina hiyo,walibainisha  kuwa mambo mengi hasa jinsi ya kuchukua hatua za haraka wakati wa moto na kuwa tayari zaidi kuweza kukabiliana na majanga ya Moto baada ya Semina hiyo.

Semina hii imekuwa ni hatua muhimu kwa UDART katika kuimarisha usalama na utayari wa wafanyakazi wake. Mbali na mafunzo ya kukabiliana na moto, semina za namna hii zinaimarisha pia uelewa wa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuepuka matukio ya moto na jinsi ya kuchukua hatua za kuzuia matatizo kabla hayajatokea.

Semina hii imeonyesha dhamira ya UDART katika kuhakikisha kuwa inawajengea uwezo wafanyakazi wake kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kuzima moto na usalama kazini. Hatua hii inategemewa kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha utendaji na usalama wa shughuli za kila siku za kampuni.Hii imepokelewa vizuri na washiriki na inaonyesha mwelekeo mzuri wa UDART katika kuendelea kuwekeza katika mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake. Wafanyakazi wengi wamejitolea kujifunza zaidi na kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata kwa manufaa ya kampuni na jamii kwa ujumla.

Share With Friends

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

Recent Posts

Scroll to Top