UDART

UDA RAPID TRANSIT PLC

UDA RAPID TRANSIT PLC

Alert GIF Semina Ya Kufunga Mwaka 2024, Na Kuangazia Maboresho Ya Huduma Bora Kwa Wateja Kwa Mwaka Ujao 2025.

MKURUGENZI MKUU wa kampuni ya mabasi yaendayo haraka UDART Ndg. Waziri Kindamba aliitisha semina ya Maboresho kwa wateja katika utoaji wa huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka siku ya tarehe 05/12/2024 ikiwa ni moja ya sehemu ya semina za mafunzo katika kukumbushana misingi bora ya utoaji wa huduma nzuri za usafiri kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Katika semina hiyo MKURUGENZI MKUU aliwaalika taasisi na wadau mbalimbali katika huduma za mabasi yaendayo haraka wakiwemo Viongozi waandamizi na wakufunzi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, na Maofisa kutoka Wakala wa Usimamizi wa Miundombinu-Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, DART.

Semina hiyo iliyoitishwa na MKURUGENZI MKUU ilikuwa pia na lengo la kuimarisha mahusiano bora kati ya Kampuni ya UDART, na Taasisi wadau wa huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.

Hakika semina hiyo ilitoa wasaa mzuri kwa Wakufunzi na Viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani  kutoa mafunzi ya ziada kwa Madereva ili kukumbushana namna ya kuepuka changamoto za mara kwa mara barabarani na matumizi sahihi ya elimu ya udereva wa kujihami kwa madereva wa mabasi hayo.

Wakichangia hoja kwa nyakati tofauti tofauti Viongozi waandamizi na wakufunzi kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani, waliahidi kuimarisha ushirikiano  wakati wa utoaji wa huduma za usafiri za mabasi yaendayo haraka hasa katika kusaidia kutoa kipaumbele kwa mabasi yaendayo haraka kwenye makutano ya barabara hasa katika maeneo ya taa za barabarani “Fire”, Msimbazi na Magomeni Mapipa.

Imeonekana mara kadhaa mabasi hayo huchukua muda mrefu kusubiri katika foleni inayosababishwa na msongamano wa magari mengine kupishana, na kupelekea mabasi kuchelewa ratiba zake jambo ambalo hupelekea malalamiko mengi toka kwa wateja, na imekuwa kero kwa watumiaji wa usafiri wa Mabasi yaendayo haraka.

Akifunga semina hiyo MKURUGENZI MKUU wa kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART aliahidi kuendelea kuthamini umuhimu wa kuitisha semina hizo ili kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya UDART na wadau wa huduma ya usafiri huo wa umma. Semina hizo pia huwa ni wasaa mzuri kwa madereva kukumbushwa umuhimu wa kuzingatia sheria za Barabara, na mafunzo ya udereva wa kujihami ili kuongeza ufanisi wakati wa utoaji wa huduma.

Share With Friends

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

Recent Posts

Scroll to Top