UDART

UDA RAPID TRANSIT PLC

UDA RAPID TRANSIT PLC

Alert GIF Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mabasi yaendayo haraka UDART na menejimenti washiriki kutoa msaada kwa waathirika wa ajali ya kuanguka kwa jengo Kariakoo

MKURUGENZI MKUU wa Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART Ndg. Waziri Waziri Kindamba, pamoja na timu ya menejimenti ya Kampuni wameungana na wananchi kushiriki katika juhudi za kusaidia katika shughuli ya kuokoa waathirika wa jengo la ghorofa nne lililoanguka eneo la Kariakoo siku ya tarehe 16/11/2024.

Katika kuonesha mshikamano na jamii, UDART imetoa msaada wa katoni zaidi ya 500 za maji ya kunywa kama sehemu ya uwajibikaji wa kurejesha kwa jamii, msaada huo wa maji ya kunywa ulipokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Hamis Nderiananga akiambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Makwiro, ambapo msaada huo ulipokelewa kwa shukrani kubwa na timu za uokoaji, maafisa wa serikali, na wanajamii waliojitokeza kusaidia juhudi za uokoaji.

Hatua hiyo ya Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART kushiriki katika kutoa msaada wa hali na mali imeonesha dhamira ya UDART ya kuwa karibu na jamii inayoihudumia, ampapo sehemu kubwa ya wafanyakazi na wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo hutumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka kuweza kuwafikisha kwa urahisi katika majukumu yao ya kila siku.

Pia MKURUGENZI MKUU Ndg. Kindamba alisisitiza kuwa utoaji wa msaada huo una umuhimu mkubwa kwani ni sehemu ya kampuni kuweza kushiriki katika changamoto zinazoikumba jamii. Wananchi walioshuhudia tukio hilo waliipongeza UDART kwa moyo wa kujitolea na kuwahimiza wadau wengine kuiga mfano huo wa mshikamano

Share With Friends

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

Recent Posts

Scroll to Top